Necta yataja shule 10 zilizofaulu kwa ubora zaidi na kumtaja mwanafunzi aliyefanya vizuri matokeo ya kidato cna nne 2018

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, na kutaja shule 10 zilizofanya vizuri katika mtihani huo kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.
Katika matokeo hayo mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi ni kutoka shule ya sekondari Ilboru ya Arusha, anaitwa Hope Mwaibanje.
Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Januari 24, 2019 mkoani Dodoma, Katibu Mkuu wa Baraza, Dk. Charles Msonde amezitaja shule hizo kuwa ni St. Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys, Ahmes, Marian Girls (zote Pwani), Canossa, Bright Future Girls (zote Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa).
Amesema watahiniwa tisa wasichana kati ya 10 bora kitaifa, katika matokeo haya ni kutoka Shule ya Wasichana ya Mtakatifu Francis ya Mbeya, huku msichana wa 10 bora kitaifa, anatoka shule ya Wasichana ya Anwarite ya Kilimanjaro.

No comments:
Post a Comment