About Us

Sema Nasi Group ni kikundi ambacho kimeanzishwa mnamo tarehe 3 mwezi wa 10 mwaka 2018 kikiwa na lengo la kuweza kuwasaidia watu wenye uhitaji.

kama vile

  •  watoto yatima kwa kute mbelea shule mbalimbali na kuweza kutoa misaada kama vifaa vya shule .

  • wagonjwa mahosipitalini  maana tunatambua kuwa watu wengi wanashida mbalimbali hivyo basi baadhi ya jamii kushindwa kuwasaidia wagonjwa wao wakiwa mahospitalini hivyo basi kikundi hiki cha semanasi kikaona ni vyena kuwasaidia watu hao ambao wametelekezwa na amilia zao kwa kuwapatia baadhi ya mahitaji 

  • wazee  wasiojiweza ,pia kikundi cha semanasi kimeamua kuweza kuwasaidia wazee wasiojiwea ili kuweza nao kutambua kuwa wanahaki ya kuishi maana jamii nyingi zimekuwa na hali ya kuwanyanyapaa wazee na wengine kudiliki kuwaita wachawi .

  • pia moja kwa moja kikundi cha semanasi kinaelimisha jamii kutokomeza mila potofu ambazo jamii nyingi zimekuwa wakijijengea na kuamini mila hizo potofu .

Kikundi hiki cha semnasi kinapatikana Mkoani Mara Wilaya ya  Tarime Mjini pia wilaya ya Rorya 

Wazo la kuanzishwa kwa kikundi hiki cha Semanasi ni kwamba jamii nyingi zinaangaika bila kupata msaada wowote kutoka kwa familia zao .jamii kwa ujumla kuunga mkono kikundi hiki ili kuweza kuanikisha malengo na hii itasaidia kupunguza ongezeko wa watoto mitaani ,ombaomba ,kupungua wa imani za kishirikina.

Waweza wasiliana nasi kupitia 

nambari;

0658774406 (M/kiti wa kikundi SHILAZY GEORGE)

0762188404  ( Katibu wa kikundi NYAMBILI YOHANA)

 

No comments:

Post a Comment